Press enter to see results or esc to cancel.

eti nini?

Mwanadada fulani eti kaniuliza kama najua kuandika kiswahili, kisha akapata mshangao nilipomjibu kihakika. Mwenyewe anaishi Bongo, kwao haswa ni huko Tz lakini makubwa ni kwamba yeye hajui kuandika kiswahili vile.

Haidhuru. Jambo la muhimu ni kwamba amejiunga na sarakasi ya wanablogu – hata usiku wa manane – hii sasa ninazungumza nae kwenye hotmail – hii sijui live waya, sijui live nini… saa nane usiku. Janga kubwa hili.

Nenda mcheki Sahara Soul Food umpe karibu. Na ukimuona, mwambie “kwisha yeye. kaingia pangoni hajitoi”

Comments

comments

%d bloggers like this: